Rais wa Venezuela afanyxa ziara ya kushtukiza Qatar

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amewasili Qatar katika ziara ya ghafla katika taifa hilo lenye utajiri wa nishati ambalo siku za nyuma lilisaidia uchumi wa nchi yake uliodorora.Maduro alionyeshwa na Shirika la Habari la Qatar akikaribishwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Doha na Waziri wa Mambo ya Nje Sultan bin Saad Al Muraikhi.Duru za kidiplomasia zilisema kiongozi huyo wa Venezuela ambaye yuko katika ziara ya Mashariki ya Kati ya nadra kwenye jukwaa la kimataifa atakuwa Qatar kwa siku mbili.Mwishoni mwa Juma Maduro alikuwa Iran ambako alisaini mkataba wa miaka 20 wa ushirikiano na jamhuri hiyo ya Kiislamu. Alikuwa Kuwait Jumatatu na hapo kabla alikuwa Algeria na Uturuki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii