Biden kuzuru Saudi Arabia na Israel

Rais Joe Biden wa Marekani amethibitisha kufanya ziara nchini Saudi Arabia mwezi ujao kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa taifa hilo ikiwa ni hatua ya mabadiliko makubwa yanayoonesha kugeuka kwa msimamo wake kuhusu taifa hilo la kifalme.Katika ziara yake hiyo ya eneo la Mashariki ya Kati, itakayofanyika kati ya Julai 13 hadi 16 na kumfikisha hadi Israel na Ukingo wa Magharibi inatazamwa kuzima msimamo wake kuhusu Saudi Arabia inayotajwa kuwa na rekodi mbaya kuhusu haki za binaadamu.Biden atatumua muda huo kujenga vyema uhusiano uliovurugika na taifa hilo huku akijitahidi kufanya jitihada kufanikisha makubaliano ya biashara ya mafuta wakati huu ambao bei ya mafuta imepanda kwa watumiaji nchini Marekani.Nchini Saudi Arabia anatarajiwa kuzungumza na Mwanamfaleme Mohammed bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme ambae Marekani ilimtaja kuhusika na mauwaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggji huko Uturuki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii