Mahakama ya Cambodia yawatia hatiani wapinzani 60

Mahakama moja ya mji wa Phnom Penh nchini Cambodia imewakuta na hatia takriban wanasiasa 60 wa upinzani, akiwemo mwanaharakati na mksoaji mkubwa mwenye uraia wa Marekani na Cambodia Theary Seng.Hukumu hiyo dhidi ya wanasisa wengi imejiri mnamo wakati kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Hun Sen akikabiliana na upinzani kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao.Kiongozi wa upinzani Sam Rainsy ambaye amekuwa akiishi Ufaransa tangu mwaka 2016 kuepuka jela, amesema mashtaka hayo yamechochewa kisiasa. Aidha ameongezewa hukumu nyingine ya miaka mingine minane.Mwanaharakati Theary Seng alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa kosa la uhaini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii