Kipindupindu kimeibuka tena Cameroon na kusababisha vifo takribani 150

Zaidi ya watu 150 wamefariki kutokana na kuibuka tena kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Cameroon katika kipindi cha miezi minane iliyopita Umoja wa Mataifa ulisema Jumatatu.

Wizara ya afya ya Cameroon iliandikisha kesi 8,241 na vifo 154 hadi mwisho wa mwezi mei, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) ilisema.

Mikoa saba kati ya 10 ya taifa hilo la Afrika magharibi wameripoti kesi za kipindupindu. Mikoa iliyoathirika zaidi ni mikoa inayotumia lugha ya kiingereza, huko kusini-magharibi ikiwa na kesi 5,628 na vifo 90 ikifuatiwa na wilaya ya Littoral yenye kesi 2,208 na vifo 58 OCHA ilisema.

Fursa ya kufika kusini-magharibi bado ni ngumu sana baada ya miaka mingi ya ghasia kati ya watu wanaotaka kujitenga wanaotumia lugha ya Kiingereza na jeshi, alisema mkuu wa OCHA ofisi ya Cameroon, Karen Perrin.

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha ambao unatibika kwa dawa za Antibiotic na kunywa maji kwa wingi lakini ugonjwa unaweza kuua ndani ya saa chache kama usipotibiwa.

Milipuko hutokea mara kwa mara huko Cameroon ambapo kuna wakaazi zaidi ya milioni 25. Janga la mwisho la kipindupindu lilitokea kati ya Januari na Agosti mwaka 2020 ambapo watu 66 walikufa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii