INAWEZA kuwa habari ya
kushtua sana kwa mashabiki wa Yanga, lakini ndivyo ilivyo kwamba wakala
wa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, alilipelekea jina la kocha
huyo kwa mabosi wa Simba ili kumtafutia kazi mpya.
Za Ndaani
Kabisa, zinasema kuwa wakala huyo alilipelekea jina la Nabi kwa vigogo
wa Msimbazi, baada ya awali klabu hiyo kuchomoa kumchukua ilipokuwa
ikisaka kocha wa kuziba nafasi ya Sven Vandenbroeck aliyekuwa ametangaza
kuachia ngazi siku chache baada ya kuifikisha timu hiyo makundi ya Ligi
ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Taarifa hizo zinasema Simba ilimkataa Nabi na kumchukua Didier Gomes aliyekuwa amepishana na Nabi ndani ya El Merreikh ya Sudan.
Gomes
alijiondoa El Merreikh ilipotinga makundi na nafasi yake kuchukuliwa na
Nabi ambaye alikaa kwa muda mchache kabla ya kufurushwa baada ya
kuboronga makundi ikiwamo kutoka suluhu na Simba mjini Khartoom katika
mechi zao za makundi msimu huo.