Zaidi ya watu laki nane wakimbia ukame Somalia

Shirika la Umoja wa mataifa lenye kuhusika na usaidizi wa dharura OCHA limesema ukame ulioikumba Somalia umesababisha zaidi ya watu 805,000 kuyahama makazi yao hadi mwishoni mwa Mei.Rekodi zinaonesha kwa mwezi Mei pekee kumerekodiwa zaidi ya watu 33,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 28 ikilinganishwa na Aprili. Kimsingi watu wameanza kulikimbia taifa hilo kuanzia Januari 2021.Somalia na mataifa mengine yanakabiliwa katika kanda hiyo yanakabiliwa na ukame mbaya kabisa katika miongo hii, baada ya kukumbwa na ukata mvua za mwaka katika vipindi vya mfululizo.Kwa mujibu wa takwimu za serikali ukame uliodumu kwa miezi kadhaa kwa taifa hilo lenye jumla ya watu milioni 16, utaathiri zaidi ya watu milioni 6.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii