Mikhail Kassianov alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya Vladimir Putin. Lakini hata hivyo, Mikhail Kasyanov hakuweza kufikiria kiongozi wake wa zamani kweamba anaweza kufanya uvamizi dhidiu ya Ukraine.
"Putin niliyemjua alikuwa tofauti," amesema Bw. Kassianov wakati wa mahojiano, katika mkutano wa video . Mikhail Kassianov, Waziri Mkuu kuianzia mwaka 2000 hadi 2004 kabla ya kuhamia upinzani, amebaini kwamba vita vinaweza kudumu hadi miaka miwili, lakini bado anaamini kwamba Urusi itarejea kwenye "njia ya kidemokrasia" siku moja.
Akiwa na umri wa miaka 64, waziri wa zamani wa Bw. Putin, ambaye alifanya kazi kwa maelewano kati ya Moscow na nchi za Magharibi, anaeleza kwamba hakufikiria, kama Warusi wengi, kwamba vita vingelizuka.
Anaeleza kwamba hatimaye alielewa kilichojiri siku tatu kabla ya uvamizi huo, wakati Bw. Putin aliwaitisha wajumbe wa baraza lake la usalama kwa ajili ya mkutano uliotangazwa kwenye televisheni.
"Nilipotazama mkutano huo wa Baraza la Usalama la Urusi, hatimaye nilielewa kuwa ndio, kutazuka vita," amesema. “Ninawafahamu watu hawa na kuwatazama niliona kuwa Putin hakuwa peke yake katika mpango huo wa uvamizi. Sio katika suala la kiafya, bali kisiasa,” ameongeza. Alipofutwa kazi na rais Putin mwaka wa 2004, Bw. Kasyanov alijiunga na upinzani na kuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Kremlin. Sasa anaongoza Chama cha Uhuru wa Watu (Parnas), chama kidogo cha kiliberali.