Hatma ya Sakaja Kujulikana Leo

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetoa makataa kwa Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja kujibu kesi nne dhidi yake kufikia 12pm Jumatatu, Juni 13.
Uamuzi huo umetolewa na mwenyekiti wa Kamati ya Kusuluhisha Mizozo ya IEBC, Titus Tiego ambaye alikubali ombi la wakili wa Sakaja, Adrian Kamotho la kupewa muda zaidi ili kuwasilisha ushahidi huo. Seneta huyo pia anataka mmoja wa makamishna wa IEBC kujiuzulu kutoka kwa kikao hicho.
Kesi nne zilizowasilishwa dhidi ya Sakaja zilitaka kuidhinishwa kwa Seneta Sakaja na IEBC kubatilishwa kwa misingi kwama vyeti vyake vya masomo ni vya kutuliwa shaka.
"Ninaomba mahakama hii inipe muda zaidi wa kuwasilisha ombi rasmi la kutaka mmoja wa wanachama watatu wa mahakama ya IEBC ajiondoe na pia kujibu madai yaliyowasilishwa dhidi ya Sakaja," wakili huyo aliiomba mahakama hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii