Straika mpya Simba kumekucha

Mkongomani aliyeko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Simba, Ceasar Manzoki ameaga rasmi wachezaji wenzie na mashabiki wa Vipers ya Uganda.

 Simba imefanya mazungumzo na staa huyo wa DR Congo na wameshakubaliana ambapo mkataba wake unamalizika Alhamisi.

Msimu huu kwenye Ligi ya Uganda alitwaa tuzo ya ufungaji bora akiwa na mabao 18, staa wa msimu na mchezaji bora wa wachezaji. Katika ukurasa wake jana aliandika ujumbe wa kuaga akishukuru na kusema hataisahau klabu hiyo.

Mmoja wa viongozi wa Simba alidokeza kwamba mchezaji huyo ndiye mbadala wa Meddie Kagere ambaye watatemana nae. Alisema kwamba Kagere amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba lakini lazima wafanye mabadiliko magumu ili kuirejesha Simba kwenye hadhi yake ndani na nje ya Tanzania.

Tayari Simba imeshamtambulisha, Moses Phiri na habari za uhakika ni kwamba anayefuatia ni Manzoki ambaye muda wowote atakanyaga kwenye ardhi ya Tanzania. Winga Mkenya, Harrison Mwenda wameshindwa kuafikiana na amerudi kwao wakati akisikilizia simu ya Azam.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii