Korea Kaskazini yakabiliwa na mafuriko katikati ya mlipuko wa Covid-19

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vimeripoti kuwa raia wa nchi hiyo wanaendelea na juhudi za kuyalinda mazao na vifaa vyao kufuatia mvua kubwa inayonyesha nchini humo. Waangalizi wa kimataifa wameonya kuwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua hiyo yanaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mwengine wa kiuchumi katikati ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19. Mafuriko yanayotokea wakati wa kiangazi katika taifa hilo, ambalo ni moja kati ya nchi maskini barani Asia, aghalabu husababisha uharibifu mkubwa katika kilimo na sekta nyengine kutokana na miundo mbinu mibaya. Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un amesema vimbunga vilivyoambatana na mvua kubwa ni miongoni mwa janga kubwa kushuhudiwa nchini humo na ambalo limesababisha migogoro mikubwa nchini humo, pamoja na vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyowekewa nchi hiyo kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii