“Hapa kuna watu wametoa ushuhuda na mimi nataka nitoe wangu. Mimi
mwenzenu nilijiunga na EOTF mwaka 1997 nikiwa kama mmoja wa Bodi ya
Wadhamini ni kiwa kijana kisichana machachari sana lakini nilipata breki
yangu Mama Mkwizu ndiye aliyenishika mkono akaniambia wewe tulia hapa.
Nilifanya kazi pamoja na Bodi kwa miaka mitatu hadi 2000 nikaingia mambo ya siasa, na iliyoniingiza kwenye siasa ni hiyo EOTF.
Nakumbuka siku moja tulikuwa tunakwenda kuwatembelea wakina Rugimbana
kijijini kwao Chamanzi, kulikuwa na kijiji cha vijana na wakati watu
wote wanaingia kwenye magari mimi nilikuwa nimezubaa… Mama alikuwa
kwenye gari akaniona nimezubaa akaniuliza wewe Mpemba vipi nikamwambi
magari yamenikimbia akaniambia ingia humu.
Wakati niko kwenye gari akaniambi wewe unafaa uingie kwenye siasa, nika
mwambia naazia wapi akasema niulize wenzangu wameingiaje na ndipo mwaka
2000 nikaingia Baraza la Wawakilishi na baadaye Waziri, Makamu wa Rais
na sasa niko hapa.— Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Sherehe ya miaka
25 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa sawa kwa wote.