Bunge la Somalia lamuidhinisha Barre kuwa waziri mkuu mpya

Bunge la Somalia limemuidhinisha bila kupingwa Hamza Abdi Barre kuwa waziri mkuu wa 21 wa nchi hiyo. Wabunge wote 220 waliokuwemo bungeni walipiga kura na kuunga mkono uteuzi wa Barre. Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa, Barre aliliambia bunge kuwa ataunda serikali itakayolenga kuwashirikisha wote ili kuimarisha utulivu wa kisiasa. Utawala mpya nchini humo utakumbwa na changamoto kama vile njaa na mashambulizi ya wanamgambo wenye itikadi kali za kidini Alshabaab. Barre aliteuliwa mapema mwezi huu na rais Hassan Sheikh Muhamud. Mohamud mwenyewe alichaguliwa mwezi Mei baada ya uchaguzi uliocheleweshwa mara kadhaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii