Biden azungumza na rais mpya wa Colombia na kusisitiza ushirikiano

Rais wa Marekani Joe Biden amezungumza kwa simu na rais mpya wa Colombia Gustavo Petro hapo jana, na kuzungumzia ushirikiano katika masuala ya usalama, usafirishaji wa dawa za kulevya na mabadiliko ya tabianchi. Taarifa hii ni kulingana na ikulu ya White House.Biden kwenye mazungumzo hayo alijikita katika suala la ushirikiano na kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili lakini pia utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya mwaka 2016. Rais Petro, ambae ni mpiganaji wa zamani wa msituni kutoka kundi la M-19 amesema kwa kifupi tu kwamba amekuwa na majadiliano ya kirafiki na rais Biden. Petro mara kwa mara amekuwa akikosoa namna Marekani inavyoendesha vita dhidi ya dawa za kulevya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii