Rais wa Indonesia Joko Widodo kuzuru Kyiv na Moscow

Rais wa Indonesia na Mwenyekiti wa kundi la nchi G20 zilizoendelea zaidi na zinazoendelea kiuchumi, Joko Widodo, hivi karibuni atafanya ziara nchini Ukraine na Urusi kujadili athari za kiuchumi na kibinadamu za uvamizi wa Urusi, ametangaza Waziri wake wa Mambo ya Kigeni.


Rais atasafiri kwenda Kyiv na Moscow baada ya kuwakilisha Indonesia kama nchi ngeni katika mkutano wa G7 nchini Ujerumani mnamo Juni 26 na 27, amesema Retno Marsudi.

Atakuwa kiongozi wa kwanza wa bara la Asia kuzuru nchi zote mbili tangu kuanza kwa mzozo huo. "Wakati wa ziara yake mjini Kyiv na Moscow, Rais atakutana na Rais (Volodymyr) Zelensky na Rais (Vladimir) Putin," ameongeza Retno Marsudi katika mkutano na waandishi wa habari mtandaoni.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii