Mohammed bin Salman ziarani nchini Uturuki miaka minne baada ya kuuawa kwa Khashoggi

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman anatarajiwa kufanya kuzuru Uturuki Jumatano hii, Juni 22 kwa ziara ya kiserikali ambapo atapokelewa na Rais Recep Tayyip Erdogan.


Ziara hii inazima ugomvi uliotokana na mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi mjini Istanbul mnamo mwezi Oktoba 2018. Rais wa Uturuki anatarajia hasa kupata faida kubwa za kiuchumi kutokana na maridhiano haya.

Chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki, Republican People's Party au CHP, kimeamua kukosoa kwa kejeli ziara hii ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia zaidi ya miaka mitatu na nusu baada ya kuuawa kwa Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul.

"Muuaji anarudi kwenye eneo la uhalifu," Mbunge Özgür Özel ameandika kwenye Twitter, chini ya picha ya Recep Tayyip Erdoğan akimkumbatia Mohammed bin Salman.

Mnamo mwaka 2018, viongozi wa Uturuki walikuwa wameendesha kampeni ya mawasiliano ya kimataifa ikionyesha kidole juu ya jukumu la mwanamfalme Mohammed bin Salman katika kifo cha mwandishi wa habari Jamal Khashoggi. Lakini mwezi Aprili mwaka uliyopita, uamuzi wa mahakama ya Uturuki - kwa ombi la mamlaka - nchini humo kufutilia mbali kesi ya mauaji haya, ulifungua njia ya upatanisho.

Baada ya ziara ya Tayyip Erdogan mjini Riyadh miezi miwili iliyopita, kuwasili mjini Ankara kwa mtu aliyepewa jina la utani "MBS" kunathibitisha mabadiliko haya ya kidiplomasia. Rais wa Uturuki anatarajia kupata aina fulani ya msaada wa kifedha ili kukabiliana na athari za mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi ambao nchi hiyo imekuwa ikipitia kwa zaidi ya miaka 20. Mgogoro ambao unatatiza nafasi yake ya kuchaguliwa tena mnamo mwezi Juni 2023.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii