Serikali ya Ujerumani imefahamisha leo jumapili kuwa itachukua hatua za dharura ili kuhakikisha inakidhi mahitaji yake ya nishati baada ya kupungua kwa usambazaji wa gesi kutoka Urusi. Miongoni mwa hatua hizo ni kuongezeka kwa matumizi ya makaa ya mawe. Katika taarifa yake, wizara ya uchumi imebaini kuwa, ili kupunguza matumizi ya gesi, ni lazima mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe itumike zaidi badala ya gesi. Katika mahojiano yake siku ya Ijumaa na kituo cha habari cha dpa, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema anapinga kujadili "hatua moja moja" bila ya kuwepompango wa jumla utakaoidhinishwa.