Viongozi wa EU wakubaliana kuacha kuagiza asilimia 90 ya mafuta kutoka Urusi

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wamekubaliana kupiga marufuku uingizaji wa hadi theluthi mbili ya mafuta kutoka Urusi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa siku ya kwanza ya mkutano wa kilele mjini Brussels uliotawaliwa na suala la mzozo wa Ukraine. Taarifa ya makubaliano hayo imetolewa na viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa mashauriano marefu juu awamu mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi. Katika awamu ya sasa mafuruku hiyo itahusisha mafuta ya Urusi yanayosafirishwa kwa meli kuingia barani Ulaya ambayo ni sawa na asilimia 90 ya mafuta yote kutoka Moscow. Hata hivyo asilimia 10 ya mafuta yanayosafirishwa kwa kutumia bomba la Druzhba kwenda mataifa kadhaa ya katikati na mashariki mwa Ulaya hayatawekewa vikwazo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii