Biden kukutana na gavana wa Benki Kuu kujadili mfumuko wa bei

Rais wa Marekani Joe Biden leo atakutana na gavana wa benki kuu ya Marekani Jerome Powell kwa mazungumzo kuhusu hali ya uchumi wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla katika wakati mfumuko mkubwa wa bei unaongeza mzigo kwa raia wengi wa Marekani. Kikao hicho cha leo kitakuwa cha kwanza tangu Biden alipomteua Powell kuendelea na wadhifa wake wa kuiongoza benki kuu ya Marekani kwa muhula mwingine wiki chache zilizopita. Ikulu ya Marekani imesema suala la mfumuko wa bei ndiyo litakuwa ajenda ya juu ya mashauriano kati ya Biden na Gavana huyo wakilenga kutafuta njia za kuimarisha uchumi wa Marekani. Mapema mwaka huu kiwango cha mfumuko wa bei nchini Marekani kilivunja rikodi ya miaka 40 baada ya kutokea mparaganyiko wa mifumo ya usambazaji bidhaa duniani uliochochewa na janga la virusi vya coorna na hivi karibuni vita kati ya Urusi na Ukraine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii