Hii ina wahusu madereva, Basi tangazo hili kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) linakuhusu sana. Iko hivi, Latra imetangaza kuwa kuanzia sasa itaanza kuwatahini madereva wa magari yanayotoa huduma za usafiri kibiashara na utaratibu huo utaanza rasmi Juni Mosi, 2022.
Miongoni mwa madereva watakaohusika ni pamoja na wa mabasi ya mikoani, daladala, wa teksi, malori makubwa yanayotoa huduma zake ndani na nje ya Tanzania.
Hata hivyo, huenda tangazo hilo lisiwahusu madereva wa bodaboda na bajaji kwa kuwa usimamizi wao kwa sasa hauko chini ya Latra.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumatatu Mei 30, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe imesema uthibitisho huo utafanyika kwa mfumo wa kielektroniki.
“Kwa mujibu wa Kifungu Na. 5(1) (e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, 2019, Mamlaka ina jukumu la kusajili wahudumu na kuthibitisha madereva wa magari yanayotoa huduma za usafiri kibiashara,” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tayari Latra imetengeneza mfumo wa kielektroniki ambao utatumika kuwatahini na kuwathibitisha madereva hao.
“Katika kutekeleza jukumu hilo kisheria, Mamlaka imetengeneza mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuwatahini madereva wa magari yanayotoa huduma za usafiri kibiashara kwa lengo la kuwathibitisha. Hivyo, madereva wote wanatakiwa kutuma maombi ili kupata nafasi ya kufanya mtihani huo na baadaye kuthibitishwa.
“Mamlaka inawatangazia madereva wote wa magari yanayotoa huduma za usafiri kibiashara kuwa; kuanzia tarehe 1 Juni, 2022 itaanza rasmi kutekeleza jukumu hilo” imesema taarifa hiyo na kuongeza.
Ili kuweza kujisajiliwa kwa ajili ya kuthibitishwa, dereva unapaswa kutuma maombi kielektroniki