China yashindwa kuyashawishi mataifa ya Pasifiki

China leo imeshindwa katika mpango wake wa kutaka mataifa 10 ya Pasifiki yaunge mkono makubaliano yanayojumuisha kila kitu kuanzia usalama hadi uvuvi baada ya baadhi ya nchi katika eneo hilo kuelezea mashaka makubwa. Lakini kulingana na waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi ambaye alikuwa ziarani Fiji kufanya mkutano na mataifa 10 ya visiwa katika eneo hilo, China imepata ushindi kwenye baadhi ya sehemu katika mpango wake huo. Katika mkutano na waandishi wa habari, Yi na waziri mwenzake wa mambo ya nje kutoka Fiji Frank Bainimarama, walizungumza kwa hadi nusu saa kisha wakaondoka ghafla bila kujibu maswali ya waandishi wa habari. Hatua hiyo imesababisha mengi yaliyotokea katika mkutano huo kutowekwa wazi. Jumuia ya kimataifa imekuwa ikihofia malengo ya China ya kiuchumi na kijeshi katika eneo hilo, ila raia wengi wa Fiji wanaona kwamba wananufaika na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni pasipo kujali wanapotokea wawekezaji hao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii