Korea Kaskazini yajadili kulegeza masharti ya kukabiliana na UVIKO-19

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekutana na maafisa wake wa ngazi ya juu kujadili kile kinachotazawa kama hatua ya kutaka kupunguza masharti ya kukabiliana na mripuko wa janga la virusi vya corona.Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, limesema viongozi hao wamefanya tathmini chanya ya hali ya kulidhibiti janga hilo na kufanya maboresho kwa taifa zima.Mkutano huo unatoa ishara kwamba Korea Kaskazini itapunguza makali ya sheria kali za kukabliana na janga hilo, ambazo ziliwekwa baada ya mwezi huu serikali kubaini uwepo wa mripuko wa virusi aina ya Omicron, huku taifa hilo likikabiliwa pia na mashaka ya uhaba wa chakula na hali ngumu ya kiuchumi.Duru zinasema Korea Kaskazini ina jumla ya watu 89,000 walioambukizwa. Hadi juzi Ijumaa, idadi ya waliokufa kutokana na UVIKO-19 walikuwa watu 67.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii