Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea
mapendekezo kutoka kwa wananchi wa tarafa za Loliondo, Ngorongoro na
Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo.
Mapendekezo
hayo yamewasilishwa kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma na wawakilishi wa
wakazi wa wilaya hiyo wakiwemo mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai,
Malaigwanani, Madiwani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa wanawake na
vijana.
Baada ya kupokea mapendezo hayo, Waziri Mkuu Majaliwa
amewasisitiza wananchi hao waendelee kuiamini serikali kwani haiwezi
kuwa na mipango mibovu kwa wananchi wake.
Akizungumzia kuhusu
eneo la Msomera lililoko wilayani Handeni mkoani Tanga ambako
yanaandaliwa makazi kwa ajili ya kuwahamishia wakazi wa Ngorongoro
waliokubali kuhama kwa hiari amesema, ujenzi unandelea vizuri.
Amesema
ujenzi wa nyumba za makazi 103 upo mbioni kukamilika na pia serikali
imepanga kuongeza nyumba nyingine lengo likiwa ni kufikia nyumba 500 kwa
ajili ya wakazi hao.