Korea Kusini kuboresha uwezo wa ulinzi kukabiliana na vitisho vya Kaskazini

Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini Lee Jong-sup amesema leo kwamba nchi yake itaboresha uwezo wake wa ulinzi na kufanya kazi kwa karibu na Marekani na Japan kukabiliana na tishio la nyuklia na makombora la Korea Kaskazini. Akizungumza katika mkutano wa usalama wa Asia huko Singapore, Lee amesema hali katika rasi ya Korea inaleta tishio la kimataifa na kuihimiza Korea Kaskazini kusitisha mara moja mipango yake ya silaha za nyuklia na makombora. Lee amesema nchi yake iko tayari kutoa msaada wa kiuchumi kwa Korea Kaskazini iwapo itasitisha mpango wake wa nyuklia.Marekani ilionya mwezi huu kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la saba la nyuklia, na kusema iwapo hilo litatokea, itashinikiza tena vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii