Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu
Tawala wa Mkoa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora kuwasimamisha kazi Afisa
Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, Bi Magreth Bukuku na Mkaguzi
wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, Bw. Dickson Sabe kuanzia
tarehe 11 Juni 2022 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Bashungwa
amechukua hatua hiyo wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya
Karagwe Mkoani Kagera na kubaini ucheleweshwaji wa ujenzi wa majengo ya
wodi ya wanaume, wodi ya wananamke, jengo la upausuaji na jengo la
kuhifadhi maiti, chanzo chake kikiwa ni afisa manunuzi na mkaguzi wa
ndani.
Bashungwa amesema Serikali ilitea kiasi cha shilingi
milioni 800 na zipo kwenye akaunti ya halmahauri kwa ajili ya ujenzi wa
majengo manne lakini Afisa manunuzi amekuwa na michakato isiyokuwa rasmi
na kuomba kupewa fedha ili atoe tenda kwa wazabuni na kuchelewa kufanya
maamuzi ya ununuzi wa vifaa.
“Fedha zipo kwenye akaunti, sehemu
ya tatizo ni Afisa manunuzi anapenda michakato na kuweka urasimu ili
mzabuni ajiongeze ndio afanye maamuzi kwahiyo akae pembeni uchunguzi
ufanyike kulingana na taratibu za kiutumishi” amesema Bashungwa
Aidha,
Bashungwa amesema Mkaguzi wa ndani ya halmashari amekuwa akishiriki
kusambaza vifaa katika miradi ikiwa ni pamoja ujenzi wa majengo ya
hospitali ya wilaya badala ya kusimamia thamani fedha zinazoletwa katika
halmashauri hiyo.
Wakati huo huo, Bashungwa amewaagiza
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhahikisha wanakamilisha miradi
yote ya ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya, zahanati na hospitali
za Wilaya ambayo mwisho wa utekelezaji (deadline) ni Juni 30 ilikuwa
ikitekelezwa kabla ya fedha za Mapambano na Ustawi wa Taifa dhidi ya
UVIKO- 19.
Nae, Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge
amesemea katika eneo la mradi hakuna vifaa vya ujenzi kama matofari,
mchanga na vifaa vingine ambayo vinachangia kuchelewa kwa ujenzi wa
majengo