BINGWA LIGI KUU KUONDOKA NA MILIONI 600

BINGWA wa ligi kuu tanzania bara msimu wa 2021/2022 atajinyakulia kombe la shilingi milioni 600.


Afisa mtendaji wa mkuu wa bodi ya ligi kuu [TPLB] , Almasi Kasongo , amesema kuwa leo fedha hizo ni kutokana na mdhamini wa haki za matangazo wa ligi hizo , Azam TV  na mdhamini wa liigi kuu , benki ya NBC.


  Amesema Azam TV itatoa shilingi 500 kwa bingwa , wakati NBC itamzawadia bingwa shilingi milioni 100, mshindi wa pili atapata shilingi milioni 300, ikiwa ni azam tv itapata shilingi 250 na NBC shilingi 50 huku mshindi wa tatu atapata shilingi 255 ,  ikiwa ni Azam TV ni 225 na mshindi wa NBC shilingi milioni 30. na pia NBC itatoa zawadi ya shilingi 20 kwa timu yenye nidhamu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii