Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa wakiambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na Balozi wa
Marekani hapa nchini leo Juni 8, 2022 wamekutana jijini Dar es salaam na
kujadili masuala mbali mbali ya sekta za ikiwa ni pa moja na ujio wa
msanii mashuhuri wa uchoraji ,Ashley Collins hapa nchini.
Wakizungumza
katika kikao hicho ambacho Mhe. Balozi wa Marekani nchini Tanzania
Dkt. Donald Wright ameambatana na Afisa Uhusiano wa Ubalozi huo, James
Rodriguez wamejadili pia ujio wa Timu ya wachezaji nguli wanawake ya
mchezo wa kikapu wa ligi ya NBA nchini Marekani hapa nchini ambao
watakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji wanawake wa
mchezo huo hapa nchini.
Mhe. Mchengerwa amesema viongozi hao
wamekubaliana kuendeleza malengo ya Royal Tour kwa kushirikiana zaidi
kwenye kuendeleza sekta za sanaa na michezo ikiwemo kuendeleza filamu
za hapa nchini za “Swahiliwood” ili ziwe katika kiwango cha kimataifa
kama zile za nchini Marekani kwa kupata walaam ambao watasaidia katika
maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada (script)
Amesema
Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo ya kipekee ya kuchezea filamu
ambazo zingeweza kuwa bora na kusisitiza kuwa ni azma ya serikali
kujenga mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuangalia kodi mbalimbali
ili kuwavutia wageni kuja kurekodia hapa nchini.
Aidha amesema
eneo jingine ambalo limejadiliwa ni pamoja na kutoa mafunzo maalum
katika eneo la haki miliki na hakishiriki kwa kazi mbalimbali za wasanii
ikiwa ni pamoja na tuzo za muziki na Kwa upande mwingine amesema
wamejadili namna ya kushirikisha wataalam kwenye program maalum ya
kuibua vipaji vya wasanii na wanamichezo ya mtaa kwa mtaa.