Urais Yanga...Ni jeuri ya pesa

 Vita ya nafasi ya Urais wa Yanga imeanza. Kuna majina makubwa kwa mashabiki na wanachama ambayo kabla kesho Jua halijazama yatapishana kuchukua fomu za nafasi hiyo.

Tayari ratiba ya uchaguzi huo chini ya Mwenyekiti, Malangwe Mchungahela inaonyesha zoezi hilo la kuchukua fomu litafikia tamati kesho Juni 9 likianzia Juni 5 na uchaguzi unafanyika Julai 10 mwaka huu.

Hatua ambayo itawaibua wagombea wengi leo na kesho kupishana kuziwahi fomu hizo ingawa baadhi walipanga kufanya kama sapraizi kwani siku nyingi hawajaonekana Jangwani.

Mwanaspoti limebaini kuna vikao vingi vinaendelea jijini Dar es Salaam vya kupanga mikakati huku baadhi ya wanaopanga kuchukua fomu wakitanguliza wapambe matawini kupima upepo lakini wanachunguza chini chini kujua nani mwenye nia ya kugombea hasa nafasi ya urais.

Karata hizo zinachezwa kiakili na kuna majina makubwa sita ambayo yanaviziana kuchukua fomu kuwania kiti hicho ingawa baadhi yao wapambe wao wameanza kuwanadi chinichini na kuhamasishana kujaa Jangwani siku ya kuchukua fomu.

Dk Mshindo Msolla amewaambia watu wake wa karibu lazima awanie tena kuendeleza mafanikio yake ya msimu huu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii