Wizara ya Afya imesema idadi ya maambukizi mapya ya Ugonjwa wa Virusi
vya Uviko-19 imeongezeka na kufikia 161 ikilinganishwa na maambukizi 68
kwa kipindi cha Aprili 2 hadi Mei 4, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa jana na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichwale
imeeleza kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 137, hali inayoashiria
kuwa maambukizi yameanza kuongezeka kwa jamii.
Imeeleza katika kipindi cha miezi miwili mfululizo hakuna kifo kilichoripotiwa.
"Mchanganuo
wa idadi ya waliothibitika katika kipindi cha Mei 5 hadi Juni 3, 2022
inaonesha kuwa Dar es Salaam uliripoti visa 130, Arusha (10), Mwanza
(5), Shinyanga (4), Mtwara (3), Dodoma (2), Mara (2), Morogoro (1),
Simiyu (1), Katavi (1), Kilimanjaro (1) na Mbeya (1), jumla ya wagonjwa
watatu (3) waliothibitika kuwa na Covid-19 walilazwa na wote walikuwa
hawajapata chanjo.
"Kwa takwimu hizi, inaonyesha kuwa, chanjo ni
kinga dhidi ya madhara ya uviko-19, Serikali imeendelea kutoa huduma za
chanjo nchini ili kuwezesha wananchi kupata kinga dhidi ya ugonjwa huu.
"Kuanzia
Mei 5 hadi Mei 3 Juni 2022 jumla ya wananchi waliopata dozi kamili ya
chanjo ya uviko-19 19 ni 775,680, Wizara inaendelea kuwasisitiza
wananchi kupata na kukamilisha dozi za chanjo ili kuzuia kupata ugonjwa "
Dk Sichwale