KARIM BENZEMA AZUA MSALA

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, ametiwa hatiani kwa njama ya vitisho dhidi ya aliyekuwa mchezaji mwenza wa timu ya Ufaransa Mathieu Valbuena kuhusiana na kanda ya video ya ngono. Mahakama moja ya Versailles ilimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kilichosimamishwa pamoja na amri ya kulipa faini ya dola 84,150. Malumbano ya kisheria kuhusiana na kesi hiyo yalianza mnamo 2015. Wakili wa Benzema Hugus Vigier, amesema mteja wake amechoshwa na mchakato huo. Vigier ameongeza kuwa hatua hiyo haimaanishi kwamba Benzema alihusika katika kumtisha Valbuena.Benzema alishtakiwa kwa kula njama na watu wengine ili kumshinikiza Valbuena kuhusu video ya ngono iliyoibwa kwenye simu yake.Benzema hakuichezea timu ya Ufaransa kwa miaka mitano baada ya kashfa hiyo lakini aliitwa tena kwenye mashindano ya Euro 2020 yaliyocheleweshwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii