Serikali ipo mbioni kuandaa kuani za kudhibiti bei za dawa nchini na tayari rasimu ya kanuni hizo zimeshawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alipokuwa
akijibu swali lilioulizwa na Mheshimiwa. Mhandisi Mwanaisha Ng’anzi
Ulenge (Mbunge Viti Maalum) Bungeni, Jijini Dodoma.
Mhe. Ulenge amehoji Serikali ina mpango gani wa kutoa bei elekezi ya vifaa vya tiba haswa akilenga vya macho, pua na koo.
Akijibu
Kuhusu Vifaa tiba, Dkt. Mollel amesema kuwa bei elekezi za vifaatiba
zitaandaliwa mara tuu baada ya kukamilika kwa kanuni za bei za dawa
elekezi.