Korea Kaskazini kujaribu kombora wakati Biden akiizuru Korea Kusini

Maafisa wa serikali ya Korea Kusini na Marekani wanasema Korea Kaskazini inaonekana kujiandaa kufanya jaribio la kombora la masafa marefu lenye uwezo wa kutoka bara moja hadi jengine kuelekea ziara ya kwanza kabisa ya Rais Joe Biden nchini Korea Kusini. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Seoul, naibu mshauri wa usalama wa kitaifa wa Korea Kusini Kim Tae-hyo amesema iwapo kutakuwa na uchokozi wowote wa Korea Kaskazini wakati wa mkutano huo wa kilele basi wamejiandaa kujibu. Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutambulishwa amesema taarifa za kijasusi za hivi karibuni zinaonyesha kwamba Korea Kaskazini huenda ikafanya jaribio hilo kesho Alhamisi au Ijumaa. Biden anatarajiwa kuwasili Korea Kusini siku ya Ijumaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii