Umoja wa mataifa umesema idadi ya watoto wanaokabiliwa na utapia mlo inazidi kuongezeka kidunia, hali hii ikichangiwa na janga la Uviko 19, mabadiliko ya tabia nchi na mizozo ya mataifa mbalimbali.
Shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia watoto, Unicef, limesema hali inaendelea kuwa mbaya Zaidi kutoka na kupanda kwa bei ya vyakula duniani.
Shirika hilo limetolea mifano mataifa ya pembe ya Africa na taifa la Afghanistan, kuwa miongoni mwa mataifa yalioathiika Zaidi.
Nchini Afghanistan, Zaidi ya watoto millioni moja wapo katika hatari ya kukumbwa na utapilia mlo, idadi hii ikiwa mara mbili Zaidi ikilinganishwa na mwaka 2018.
Katika mataifa ya pembe ya Afica Unicef,inasema idadi ya watoto walio katika hatari ni Zaidi ya millioni 2.