Ujerumani iko tayari Finland na Sweden ziidhinishwe katika NATO

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema nchi yake imefanya maandalizi yote ya mchakato wa uidhinishaji wa haraka iwapo Finland na Sweden zitaamua kuomba uanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO huku akisisitiza hitaji la mataifa hayo mawili la dhamana ya usalama. Akizungumza na wanahabari jana mjini Berlin, katika siku ya pili ya mazungumzo na wenzake katika Jumuiya ya NATO, Baerbock aliongeza kuwa mawaziri hao waliafikia makubaliano na kwamba hakupaswi kuwa na muda wa kucheleweshwa kutoka wakati wa kutuma maombi kwa mataifa hayo mawili ya Finland na Sweden na wakati wa kujiunga na Jumuiya hiyo ya NATO. Baerbock alikuwa anazungumzia kipindi cha uidhinishaji ambacho kinaweza kufikia hata mwaka mmoja, ambapo nchi za kanda ya Nordic hazitaweza kulindwa na kifungu cha 5 cha NATO ambacho kinahakikisha kwamba kushambuliwa kwa mshirika mmoja ni shambulio kwa wote.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii