Duterte amkosoa Putin kuhusu uvamizi nchini Ukraine

Rais wa Ufilipino anayeondoka madarakani Rodrigo Duterte, amemkosoa vikali kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kwa mauaji ya raia wasio na hatia nchini Ukraine, akisema wakati wote wawili wakitajwa kuwa wauaji, yeye anauwa wahalifu na wala sio watoto na wazee. Duterte, ambaye amemwita wazi Putin kuwa rafiki, kwa mara ya kwanza, amekemea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wakati wa mkutano wa kila wiki na maafisa wakuu wa baraza la mawaziri unaopeperushwa kupitia televisheni ambapo alilaumu vita hivyo ambavyo vimedumu kwa miezi mitatu kwa kupanda kwa bei ya mafuta duniani ambako kumeathiri nchi nyingi, ikiwemo Ufilipino. Huku akisisitiza kuwa hamlaani rais huyo wa Urusi, Duterte hakubaliani na kauli ya Putin ya uvamizi huo kuwa operesheni maalum ya kijeshi na kusema ni vita kamili vilivyoanzishwa dhidi ya taifa huru.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii