Waziri wa Usalama Uganda" Watu Maskini Hawatakwenda Mbinguni".

Waziri wa Masuala ya Ndani nchini Uganda anadai kuwa watu maskini hawataenda mbinguni kwa sababu wanamtukana Mungu kupitia malalamishi na shutuma kila siku.
Kulingana na mwanasiasa huyo, utajiri ni utukufu na kila mtu alipewa na Mwenyezi Mungu alimpa kila mja zana za kumaliza umaskini.
"Watu maskini hawataenda mbinguni kwa sababu wanamtukana Mungu kupitia kulalamika na shutuma kila siku. Mbona umsumbue Mungu kila siku ukimuomba pesa ilhali alikuwa mikono, macho, akili, shamba na mvua? "akasema Otafiire kama alivyonukuliwa na Gazeti la New Vision la Uganda.
Waziri huyo alisema kuna baadhi ya watu hawataki kufanya kazi ilhali wanataka kuwa matajiri.
"Ikiwa hutumii zana alizokupa Mungu, usimlaumu unaposalia kuwa maskini. Jitahidi kuushinda umaskini kwa sababu kuwa tajiri ni utukufu," aliongeza.
Aliwaomba Waganda kuwa na umoja na kushinikiza maendeleo badala ya kubaguana kikabila na kidini.
Vile vile Otafiire aliwashauri wazazi kuwekeza katika elimu kwani ndio msingi wa maendeleo kitaifa na kimataifa.
Ukosefu mkubwa wa ajira Uganda
Uganda inakumbana na ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana ambao ni moja ya idadi kubwa ya watu changa zaidi duniani kwa 75% ya raia chini ya umri wa miaka 30.
Haya yanajiri huku Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisema kuwa serikali yake haitaingilia kati hali ya sasa ya kiuchumi na kupanda kwa gharama ya maishi nchini humo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii