Volodymyr Zelensky kuhutubia viongozi wa dunia Davos

 Rais wa Ukraine anaendelea na ziara yake kupitia mkutano kwa njia ya video na viongozi wa dunia. Volodymyr Zelensky atahutubia Jumatatu hii Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), ambalo linakutana tena huko Davos baada ya kusitishwa kwa miaka miwili kutokana na janga Covid-19. Rias Volodymyr Zelensky atapata fursa katika jukwaa hili kuomba msaada zaidi, kifedha na kijeshi.
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umeongeza idadi ya watu waliotoroka makazi yao kufikia milioni 100 kwa mara ya kwanza, Umoja wa Mataifa umeonya Jumatatu hii.
"Idadi ya watu waliolazimika kukimbia migogoro, ghasia, ukiukwaji wa haki za binadamu na mateso imepita kiwango cha milioni 100 kwa mara ya kwanza, kutokana na vita vya Ukraine na migogoro mingine mibaya" shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi UNHCR limesema  katika taarifa.
Rais wa Marekani Joe Biden alisema mnamo Mei 23 mjini Tokyo kwamba Urusi "lazima ihukumiwe" kwa "unyama wake wa kishenzi nchini Ukraine" katika suala la vikwazo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake. "Sio tu kuhusu Ukraine," Biden alisema. Kwa sababu ikiwa "vikwazo havitadumishwa katika mambo mengi, basi hiyo itatuma ishara kwa China kuhusu gharama ya jaribio la kuichukua Taiwan kwa nguvu? alijiuliza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii