IMF yataka serikali zitoe ruzuku kugharamia 'makali ya maisha' kwa wananchi wake

Serikali za mataifa duniani zinatakiwa kutoa ruzuku kwa ajili ya gharama ya chakula na nishati kwa watu maskini zaidi katika jamii, mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Watu kote ulimwenguni wanakabiliwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kristalina Georgieva alisema msaada unahitajika kutolewa "kwa njia iliyolengwa sana, ikiwezekana kwa kutoa ruzuku moja kwa moja kwa watu". Serikali nyingi zinatoa msaada lakini wakosoaji wanahoji kuwa haitoshi.

Linapokuja suala la gharama ya maisha magumu, Bi Georgieva alisema: "Kuna vipaumbele viwili, kimoja watu maskini sana, makundi ya jamii ambayo sasa yanakabiliwa na bei kubwa ya chakula na nishati". Pili, aliongeza, ni kusaidia biashara ambazo "zimeharibiwa zaidi" na vita vya Ukraine.

Moja ya jukumu kubwa la IMF ni kufanya kazi na serikali z amataifa mbalimbali kuleta utulivu wa uchumi wa dunia na kuimarisha ustawi wa jamii. Hata hivyo, hilo linaonekana kuwa gumu kwa sababu bei za vyakula zimepanda na kuweka rekodi mwaka huu, wakati bei ya mafuta na gesi pia imepanda kwa kasi.

Kundi la mashirika ya maendeleo ya kimataifa ikiwa ni pamoja na IMF na Benki ya Dunia wiki hii walizindua mpango mkubwa wa kujaribu kukabiliana na uhaba wa chakula duniani kote.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii