Ukraine yakataa kusalimisha ardhi yake kwa Warusi kwenye mpango wa makubaliano ya amani

Serikali ya Ukraine inasema haitakubali makubaliano ya kusitisha mapigano na Urusi ambayo yanahusisha kuachia eneo - katika hali inayoonekana kuwa ngumu kwa msimamo wake.

Mshauri wa rais Mykhaylo Podolyak alisema Kyiv haitafuata wito wa nchi za Magharibi wa kusitishwa kwa dharura kwa mapigano ambayo yanahusisha vikosi vya Urusi vilivyosalia katika eneo wanalokalia kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

Alisema kufanya makubaliano kutasababisha Moscow kuanza mashambulizi makubwa zaidi na ya umwagaji damu katika muda mrefu zaidi. Maoni yake yanakuja huku Urusi ikiendelea na majaribio yake ya kuzingira vikosi vya Ukraine vinavyolinda mji wa mashariki wa Severodonetsk.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii