Israel yaripoti kisa cha kwanza cha homa ya nyani

Kisa cha kwanza cha homa ya nyani kimegunduliwa nchini Israel kwa mtu aliyerejea kutoka nje ya nchi. Mamlaka nchini humo zinachunguza visa vingine vinavyoshukiwa kuwa vya homa hiyo. Wizara ya Afya ya Israel imefahamisha kuwa mtu huyo amelazwa katika hospitali ya Tel Aviv na anaendelea vyema. Hata hivyo wizara hiyo imetoa wito kwa mtu yeyote anayerejea kutoka nje ya nchi akiwa na homa na vidonda kumuona mara moja daktari. Kisa cha Israel kinaweza kuwa cha kwanza kutambuliwa Mashariki ya Kati. Shirika la Afya Ulimwenguni limegundua takribani visa 80 duniani kote huku kukishukiwa kesi takriban 50. Kwa kawaida visa vya ugonjwa huu unaoshabihiana na ndui huripotiwa kwa watu wenye uhusiano na eneo la Afrika ya Kati na Magharibi lakini nchi kadhaa za Ulaya na Marekani zimeripoti visa kwa watu ambao hawakusafiri hivi karibuni barani Afrika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii