Ugonjwa wa Homa ya Nyani wasambaa duniani

Mataifa kadhaa duniani yamethibitisha maambukizo ya homa ya nyani siku kadhaa tangu Uingereza ilipotangaza mripuko wa maradhi hayo yanayosababishwa na virusi kutoka kwa wanyama wa mwituni wakiwemo nyani na kima. Hii leo Italia na Sweden zimetangaza visa vya kwanza vya ugonjwa huo ambao husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia njia ya hewa, majimaji ya mwilini au kutumia vifaa vya mtu aliyeambukizwa. Ufaransa, Canada, Marekani, Ureno, Uhispania Ubelgiji na Australia pia zimethibitisha kuwa na visa kadhaa vya maambukizo ya homa hiyo ambayo iligundulika kwa mara ya kwanza duniani mnamo mwaka 1970. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa limezitaka mamlaka za afya ulimwenguni kuchukua hatua kali za kuwafuatilia watu waliokutana na wagonjwa wa homa ya nyani na kuwatenga haraka wale watakaobainika kuwa na dalili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii