Ndovu 70 wafariki kutokana na ukame

Waziri wa Utali nchini Kenya, Najib Balala alisema kwamba Zaidi ya ndovu 70 wamefariki nchini humo, kutokana ukame ambao unashuhudiwa kanda ya Africa Mashariki, kwa kipindi cha mwaka moja.

Matangazo ya kibiashara

Ndovu waliofariki kwa mjibu wa Balala, ni wale waliokuwa katika mbuga ya kitaifa ya Tsavo, Balala akihofia kuwa ndovu Zaidi huenda wakafariki iwapo hali ya kiangazi itaendelea, huku akidokeza kuwa twiga kadhaa pia wamefariki.

Hata hivyo Balala amesema serikali inalenga kutumia bwawa moja ndani ya mbuga hiyo kuwapa wanyama pori maji ili kuzuia maafa Zaidi.

Kiangazi kanda ya Africa mashariki pia kimeathiri raia wa mataifa ya Kenya, Somalia na Ethiopia, yakitajwa kuathirika Zaidi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii