Miss Tanzania namba mbili, Juliana Rugumisa ambaye aliteuliwa kushiriki Miss World baada ya aliyeshika nafasi ya kwanza, Rose Manfere kuenguliwa kutokana na utovu wa nidhamu hatimaye amepata viza ya kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo yatakayofanyika San Juan, Puerto Rico Desemba 16, 2021
Taarifa ya kupatikana kwa visa hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 4,2021 na kamati ya Misa Tanzania kupigia ukurasa wao wa Instagram..
Kuhusu kuchelewa siku ya mwisho ya kuingia kambini iliyokuwa jana Desemba 3, waandaaji hao wameeleza kuwa wanafanya mawasiliano na uongozi wa Miss World na watatoa taarifa rasmi.