Mwanaanga wa Kijerumani Matthias Maurer yuko njiani kurejea duniani baada ya karibu miezi sita kuwepo angani kwenye kituo cha anga ya kimataifa. Maurer na wenzake watatu kutoka Marekani wakiwa katika chombo chao wameonekana katika taswira za Shirika la taifa la Marekani linaloshughulikia utafiti wa anga za mbali NASA.Chombo chao kinatarajiwa kutua katika eneo la bahari karibu na pwani ya Florida huko Marekani. Endapo kila kitu kitaenda kulingana na mpango ulivyo, Maurer anatarajiwa kuwasili Ujerumani kesho jioni.Anatarajiwa kushukia katika sehemu ya uwanja wa ndege wa kijeshi ya uwanja wa Cologne/Bonn. Muuer ambae anatoka katika jimbo la magharibi mwa Ujerumani la Saarland, alifanya safari ya kwenye anga ya kimataifa na wenzake watatu Novemba 11 mwaka uliopita. Anakuwa Mjerumani wa 12 kufika katika hatua hiyo.