Waziri Mkuu wa India ziarani barani Ulaya

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi leo anaanzia ziara yake barani Ulaya kwa kuzitembelea Ujerumani, Denmark na Ufaransa huku uamuzi wa serikali yake wa kukataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unatarajiwa kuwa ajenda muhimu ya majadiliano. Akizungumza kabla ya kuabiri ndege mjini New Delhi, Modi amesema analenga kutumia ziara yake kuimarisha ari ya ushirikiano na mataifa ya Ulaya katika wakati kanda hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi. Hii leo Modi amepangiwa kuwa na mazungumzo na kansela Olaf Scholz wa Ujerumani mjini Berlin kabla ya kuelekea Copenhagen ambako atajiunga na viongozi wa mataifa ya Scandinavia kwa mkutano wa siku mbili kati ya India na mataifa ya kanda hiyo. Kadhalika atakwenda mjini Paris kwa mkutano na rais Emmanuel Macron kujadili masuala kadhaa ya kilimwengu pamoja na ushirikiano kati ya India na Ufaransa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii