Rais wa Tunisia aahidi katiba mpya katika siku chache zijazo

Rais wa Tunisia Kais Saied amesema serikali yake itaunda kamati ya kuandika katiba mpya ya kile alichokiita "taifa jipya" nchini Tunisia. Rais Saied ameyasema haya katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni ya taifa nchini humo. Ameongeza kwamba kamati hiyo itakamilisha jukumu lake katika kipindi cha siku chache tu zijazo. Kiongozi huyo amesema mazungumzo ya kitaifa kuhusiana na mageuzi yatajumuisha mashirika 4 makuu nchini Tunisia yakiwa ni muungano wa wafanyakazi, muungano wa mawakili, shirikisho la viwanda na biashara na shirika la haki za binadamu la Tunisia. Hivi karibuni Saied alijipa nguvu ya kumteua mkuu wa tume ya uchaguzi, hatua ambayo wakosoaji wanasema inalenga kuidhoofisha tume hiyo kuelekea kura ya maoni kuhusu katiba ambayo ilikuwa imepangiwa kufanyika mwezi Julai na uchaguzi wa wabunge wa mwezi Desemba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii