Kiongozi wa Afghanistan anaye onekana kwa nadra apongeza 'usalama' katika kuadhimisha Eid

Kiongozi mkuu wa Afghanistan Hibatullah Akhundzada, ambaye alionekana hadharani leo Jumapili ikiwa ni mara ya pili tu katika kipindi cha miaka sita, amewaambia waumini waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ya Eid al-Fitr kuwa, Taliban wamepata uhuru na usalama tangu kutwaa mamlaka mwaka jana. Akizungumza siku chache baada ya bomu kulipua msikiti mmoja mjini Kabul, hali ya usalama imeimarishwa kwa kiongozi huyo aliyejumuika na maelfu ya waumini katika msikiti wa Eidgah katika mji wa kusini wa Kandahar, makao makuu ya kikundi cha Waislam wenye msimamo mkali. Makumi ya raia wameuawa katika mashambulizi yatokanayo na imani za kidini, ambayo baadhi yanadaiwa kuendeshwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS, yakilenga watu wa madhehebu ya Shia na Sufi. Mlipuko wa bomu siku ya Ijumaa katika mji mkuu Kabul uliua takriban watu 10.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii