Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi akutana na Zelenskiy mjini Kyiv

Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi akiambatana na wabunge kadhaa, amefanya ziara mjini Kyiv katika kuonyesha mshikamano kwa nchi hiyo na kuelezea matumaini kuwa ombi la Rais Joe Biden la kutoa msaada wa dola bilioni 33 kwa Ukraine litapitishwa bungeni haraka iwezekanavyo. Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ameitaka China kutoa hakikisho la usalama kwa Kyiv. Ameyasema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa hivi karibuni na vyombo vya habari vya serikali ya Beijing. Mara kadhaa, mataifa yenye nguvu ya Magharibi pamoja na Ukraine yamekuwa yakiitaka China kulaani uvamizi wa Urusi wakati nchi hiyo ikijaribu kudumisha msimamo wake inaodai hauegemei upande wowote. Marekani imetishia kuwepo kwa athari mbaya, ikiwa Beijing itatoa msaada wa kijeshi au kiuchumi kwa Moscow.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii