Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida leo hii anaanza ziara ya kuyatembelea mataifa ya kusini mashariki mwa bara Asia. Ziara hiyo itakamfikisha kwanza nchini Indonesia na baadaye atazitembelea Vietnam na Thailand. Kiongozi huyo wa Japan analenga kutafuta msimamo wa pamoja wa kanda hiyo kuhusu mzozo wa nchini Ukraine na kitisho cha kutanuka kwa nguvu na ushawishi wa China. Taarifa ya serikali mjini Tokyo imesema waziri mkuu Kishida ananuwia kuimarisha ushirikiano zaidi ili kufanikisha kanda ya bahari ya Hindi na Pasifiki kuwa eneo huru kibiashara na linalofanya kazi pamoja. Baada ya kukamilisha ziara kwenye kanda hiyo Kishida atayatembelea pia mataifa kadhaa ya Ulaya.