Biden aliomba bunge kudhinisha dola bilioni 33 kuisadia Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden ameliomba bunge la nchi hiyo kuidhinisha kitita cha dola bilioni 33 kuisadia Ukraine kupambana na Urusi. Ombi hilo linajumuisha dola bilioni 20 kwa ajili ya ulinzi wa Ukraine na washirika wa Marekani kwenye kanda ya Ulaya. Dola nyingine bilioni 8.5 zitaisadia serikali ya rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine kuendelea kutoa huduma za jamii na kuwalipa wafanyakazi mishahara. Kadhalika kuna fedha za kusaidia miradi ya kiutu duniani ikiwemo ile inayotoa msaada kwa watu waliokimbia vita nchini Ukraine. Msaada huo ambao maafisa mjini Washington wanasema utatumika kwa miezi mitano ni mkubwa kuliko ule wa dola bilioni 13 zilizoidhinishwa na bunge la Marekani mwezi uliopita. Hiyo ni ishara kwamba Marekani imedhamiria kuupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kwa muda mrefu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii