Hakuna Ambaye Amependa Toni Rudiger Kuondoka

Beki wa klabu ya Chelsea Antonio Rudiger anaondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu huu.

ANTONIO Rudiger ameamua kuondoka ndani ya kikosi cha Chelsea mwishoni mwa msimu wa 2021/22 anatajwa kujiunga na Klabu ya Real Madrid bure.

Kocha Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema kuwa hakuna mtu ambaye amependa jambo hilo litokee.

Rudiger dili lake ndani ya Chelsea linaisha muda wake mwishoni mwa msimu hivyo atakuwa huru kujiunga na timu yoyote.

Kuna orodha ndefu ya timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England zinahitaji saini ya beki huyo mwenye miaka 29 lakini anatajwa kuwa atakuwa ndani ya Bernabeu.

Tuchel amesema:”Sifikirii kwamba kama kuna mtu ambaye anapenda hili liweze kutokea lakini haya ni maamuzi yake lazima tuyakubali na kuyapokea. Tukipenda ama tusipopenda itatokea na yatakuwa na maisha lazima yaendelee,”.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii